RC MAKONDA APIGA MARUFUKU HOSPITALI KUZUIA MAITI NDANI YA MKOA WA ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda, amepiga marufuku hospitali za Mkoa wa Arusha kuzuia maiti kutokana na gharama za matibabu na badala yake zibuni njia mbadala za kudai malipo hayo.

RC Makonda ametoa katazo alipofanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli kukagua maendeleo ya Ujenzi wa jengo la mionzi na la upasuaji pamoja na kuzungumza na wahudumu wa hospitali hiyo na kuangalia namna huduma zinavyotolewa hospitalini hapo.Akiwa Hospitalini hapo , RC Makonda amewataka wahudumu wa afya mkoani Arusha kutoa huduma nzuri kwa wananchi wanaofika hospitalini na kwenye vituo vyote vya afya ili kuwa sehemu ya kuwapunguzia maumivu wananchi kutokana na magonjwa yanayowasumbua.

Sambamba na hilo, RC Makonda amesema Mkoa wa Arusha unafaa kuwa Mfano wa huduma nzuri za afya ili kuendana na uwekezaji mkubwa wa serikali ya awamu ya sita kutokana na Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fedha nyingi za kuwezesha miundombinu bora ya utoaji wa huduma za kiafya.

Huu ni muendelezo wa ziara yake ya kutembelea wilaya zote 6 mkoani Arusha aliyoipa jina la SIKU 6 ZA MOTO ARUSHA.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *