SHIRIKA LA WAKINA MAMA NA WATOTO FOUNDATION LAWAPA MKONO WA POLE WAATHIRIKA MBOZI.

Shirika lisilo la kiserikali la WAKINA MAMA NA WATOTO FOUNDATION TANZANIA Limeguswa na kutoa mchango wa vitu mbali mbali kama Sabuni,Unga pamoja na Chumvi vitu vyenye thamani ya shilingi 384,000/= kwaajili ya kuwa saidia waathirika wa Mvua kubwa ambayo iliambatana na upepo na hivyo kusababisha kuezuliwa kwa Nyumba zaidi ya 200 na kusababisha uharibufu wa baadhi ya mali ikiwemo mashamba ya mahindi na maharangwe huko Nambizo wilayani mbozi.

Akizungumza leo wakati wa kukabidhi msaada huo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mfadhili wa shirika hilo Bi.Rozina Kalupande kutoka nchini Uswizi amabaye pia ni mzaliwa wa Wilaya hiyo amesema “Nimeguswa sana na kusikitishwa sana na takio la janga hilo kwani ukiachana na msaada tuu mimi pia nimezaliwa hapa na wanapo pata tatizo wananchuii wa Mbozi ni kama limenipata mimi hivyo sisi ni kitu kimoja  na tumetoa mchango huu kidogo lakini ninahidi kutoa ushirikiano na msaada kila utakapo hitajika ili wananchi hao wajisikie faraja na wajihisi wao ni sehemu ya jamii yetu lakini kubwa ni kuwasaidia ili waweze kurudi katika shughuli zao kama mabavyo ilikuwa hapo awali” Amesema Bi. Rozina

Ameongeza kwa kusema wao kama shirika wanatambua juhudi mbali mbali zinazo fanywa na serikali ya aamu ya sita chini ya uongozi wa Rias Dkt.Samia S.Hassan hivyo hawajabaki nyuma wanatoa huduma na kuanzisha miradi  mbali mbali ili kusidia maendeleo katika jamii ikiwemo kituo cha kulelea watoto yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambao wana wanasidia mambo mbali mbali ikiwemo kuwawezesha kupama Elimu na mahitaji mbali mbali,Ujenzi wa vyoo katika shule mbali mbali,lakini pia usambazaji wa maji vijijini ili kusaidia kuepusha adha ya wakina mama na Wanawake wa vijijini kufuata maji kwa umbali mrefu ameongeza kwa kusema shirika hilo limefanikiwa kusambaza maji katika vijiji vya Namwangwa,Hezya,Haraka,Izumbi,Isite ambavyo vinapatikana wilaya ya Mbozi lakini  pia wanajishughulisha na shughuli za uchimbaji wa visima kwa kutumia mashine na mitambo maalum.

Miundo mbinu ni kitu muhimu sana katika jamii hivyo shirika hili linajihusisha pia na ujenzi wa miundo mbinu kama Madaraja ili kuweza kurahisisha zaidi shughuli za kusafirisha watu pamoja na mizizigo kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine

Mkuu wa wilaya ya Mbozi Mhe. Ester Mahawe ameshukuru kwa msaadaa huo ambao anaamini utakuwa ni mzuri na utawafaa watu walio athiriwa na mvua hizo katika wilaya hiyo hata hivyo shukrani za pekee amepeleka kwa makampuni,wadayu wa maendeleo pamoja na watu binafsi walio guswa na kutoa misaada yao ili wana Nambizo waweze kufarijika ameema serikali hii ya awamu ya sita inafanya kazi kwa ukaribu sana na wadau  mbali mbali na mashirika haya yasiyo ya kiserikali lengo likiwa ni kuleta maendelo katika jamii.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *