Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Ndg. Patrick Mwalunenge amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Jijini Mbeya kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuleta maendeleao katika jiji la mbeya na Nchi kwa ujumla Mwalunenge amewataka wananchi hao kuwa na kundi moja tu ambalo ni kundi la Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya.
Mwalunenge ameongeza kwa kusema kupitia vikao alivyo hudhuria wanaasa wana CCM kuacha makundi na majungu badala yake waungane ili kutimiza malengo na kusimamia miongozo ili kuleta maendeleo.Haijalishi ulinipigia kura ama hukunipigioa kura mimi ni mwenyekiti wa CCM na ni kiongozi wa wote huu ni muda wa kupiga kazi muda wa makundi na majungu ulisha pita mimi ni kiongozi wenu lakini pia hiki cheo ni dhamana ambayo ninyi mmenipa hivyo niko hapa kuwatumikia usiku na Mchana na si vinginevyo.
Tunataka CCM Mbeya iwe ni bustani ya Edeni na iwe nzuri na inayo meremeta kama Bustani ya Edeni hapa niwapongeze sa na madiwani kwa kazi nzuri mnayo fanya mimi kama mwenyekiti ntahakikisha kuwawekea mazingira mazuri ili mchape kazi zaidi ili kuweka mazingira ama hali ya wale walioko vyama vingine washawishike na kuja kujiunga na Chama chetu katika kuboresha mazingira hayo nimeahidi kuwagusa pia makatibu wenezi CCM ngazi ya wilaya ambapo nitawanunulia pikipiki ili waendelee kupiga kazi zaidi tuna wilaya 6 na kwenye hilil tutaanza kwanza na zile wilaya zilizoko pembezoni mwa Jiji letu.
Kwa upande wake Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ndg. Ndele Mwaselela amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuchukua hatua na uthubutu ili Chama kiendelee kupiga hatua na kupeleka maendeleo kwa wananchi amesema wako kwenye mkakati wa kuwasaidia wanachama ambao wameshaonesha nia ya kuanza ujenzi wa ofisi za Chama kwa kata na wilaya mbali mbali za jiji la Mbeya kupitia uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya
Sambamba na hilo Mwalunenge amewataka madiwani kuacha kutengeneza na kuendeleza migogoro ili wawe wamoja na kuwatumikia wananchi “Panapokuwa na migogoro ni ngumu sana sehemu hiyo kuweza kupata maendeleo na ni ngumu pia Mungu kutia baraka sehemu hiyo epukeni migogoro twendeni tukachape kazi. Amesema Ndg. Mwalunenge