RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA MWAKILISHI WA UNDP TANZANIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Bw.Shigeki Komatsubara aliyefika kujitambulisha Ikulu Zanzibar tarehe:14 Desemba 2023.

Katika mazungumzo yao wamegusia uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Zanzibar na UNDP pamoja na kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo, uchumi wa buluu, utalii, Mahakama, kujenga uwezo kwa Taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (PDB) na nyinginezo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *