Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wamewaomba wananchi radhi kutokana na kukosekana kwa huduma ya upatikanaji wa mtandao wa malipo na hivyo kufanya wananchi kupata kadhia na usumbufu katika malipo na wananchi kukosa huduma.
Shirika limesema jitihada za kurudisha huduma hiyo zinaendelea na linawataka wananchi kuvuta subla wakati utatuzi wa changamoto ukiendelea.