(RWA) KUJA NA MPANGO WA KUTOKOMEZA NDOA ZA UTOTONI.

Jukwaa la wanawake wa Vijijini (Rural Women Assembly) linalotekeleza uinuaji uwezeshaji  wanawake na kutokomeza unyanyuasaji wa kijinsia limekuja na mpango wa kutokomeza ndoa za utotoni ilikuweza kumpa zaidi nafasi binti aweza kutimiza ndoto na malango yake na hivyo kutengeneza jamii ama taifa la watu makini na uchumi imara.

Baadhi ya wanachama wa Jukwaa la Wanawake Vijijini (RWA) Wakifuatilia kwa makini elimu ya kupinga ndoa za utotoni lililotolewa katika mkutano wa wananwake kutoka mikoa ya Mbeya na Songwe Disemba,12 Mwaka huu.

RWA ni jukwaa linalo fanya kazi katika Nchi 10 zinazopatikana kusini mwa jangwa la Sahara ambazo pia ni wanachama wa Juiya ya Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika (SADC) huku Tanzania tukiwa ni moja ya wanufaika wa Jukwaa hilo Desemba 12 Mwaka huu jukwaa hili lilifanya kikao kilicho endana na kauli mbiu ya “UKIMYA NI UKATILI” kili husisha Mikoa ya Mbeya pamoja na Songwe na kuhudhuriwa na Mabinti mbali mbali na kupewa elimu ya Ukatili wa kijinsia.

Moja ya binti ambaye ni mwanachama wa jukwaa hili kutokea Wilaya ya Mbozi alitoa ushuhuda wake kwa kusema  yeye aliolewa akiwa na umri wa miaka 16 na Mwanamme ambaye hakuwa chaguo la Moyo wake hivyo Migogoro mingi ilianza kutokea,iliwemo matusi na dharau, pamoja na matumizi ya vilevi kwa mwanamme huyo. Ilipo pita muda mrefu bila mafanikio ya kupata mtoto wazazi wa mwamme walianza kumkebehi kwa kusema hana uwezo wa kupata mtoto ndipo alipo chukua uamuzi wa kuivunja Ndoa hiyo na akaolewa na mwanamme ambaye ni chaguo lake na alimpenda na mpaka saa anaishi naye.

Adivera Msukwa aliacha shule akiwa kidato cha pili alilazimishwa kuolewa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi kwa wazazi baada ya kuolewa kutokana na umri wake mdogo ilikuwa ni vigumu yeye kuweza kuhudumia ndoa hivyo alianza kusumbuana na mwanamme huyo mwaka 2017 aliachana na mwanamme huyo na kuolewa kwa mwanamme mwingine.

Mwana jukaa mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe anasema jamii kama wamasai wanafanya sana tamaduni hii ya kuwaozesha mabinti wakiwa na umri mdogo pasi na kujali kama binti ameridhia ama hajaridhia “Mimi nililazimishwa kuolewa nikiwa mdogo lakini ilipofika siku ya mwanamme kuja kunichukua nyumbani kwetu kwenda kuishi naye nilikimbia na kwenda huko porini nilikaa huko kwa takribani siku kadhaa na niripo rudi tena nyumbabni nili wasisistiza tena sitaki kuolewa wakasitisha zoezi hilo” amesema binti huyo.

Mkurugenzi wa Shirika la MIICO Bi. Catherine Mulasa akishiriki kutoa elimu ya Ndoa za utotoni katika mkutano wa jukwaa la wanawake wa vijijini (RWA) uliofanyika Disemba 12 Mwaka huu.

Catherine Mulasa Mkurugenzi wa shirika la MIICO anasema kupitia Jukwaa la RWA mabinti wanapatumia kama sehemu pekee ya kuweza kueleza changamoto pamoja na vikwazo mbali mbali wananvyo kumbana navyo katika jamii zao amesema endapo jamii tutasimama kwa umoja wetu tukakemea ndoa za utotoni itakuwa ni vizuri na tutakuwa na taifa la kizazi bora na cha watu wanao jituma kwani ukiachilia mbali elimu inayotolewa kwa mabinti hawa bado kuna faida ya kupata mafunzo mbali mbali ya kijasiriamali kama vile kutengeneza Sabuni,Vikapu,Vikoi pamoja na Shanga yatakayo wawezesha mabinti ama wanawake hawo wa Vijijini kujipatia kipato na hivyo kuimalisha hali zao za kiuchumi.

James Sambuka msimamizi wa maswala ya msaada wa kisheria nasema ndoa za utotoni ni moja kati ya ukatili wa kijinsia hivyo unapo muozesha binti mdogo pasi na ridhaa yake inakuwa ni kumfanyia unyanyasaji wa kijinsia na endapo atafanya tendo la ndoa katika ndoa hiyo itakuwa ni ubakaji. Hivyo jamii tunatakiwa kushiriki kwa pamoja kukomesha ndoa hizi ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sehemu mbali mbali kama vile katika uongozi wa serikali ya Mtaa, Kijii ama Kata Polisi,Dawati la jinsia,Maendeleo ya jamii,Mahakama. Aidha ameiasa jamii kuachana na maswala ya kimila na destuli ambazo zinachangia zaidi unyanyasaji wa kijinsia kama kuolewa katika ndoa za utotoni na kuacha kuamini imani za kishirikina “Unakuta mtu anaenda kwa mganga anapewa sharti kuwa ili afanikiwe ni lazima afanye tendo la ndoa na binti mdogo ili apate mali ama fedha kwa hiyo imani kama hizi zinachochea zaidi kuongezeka wa matukio ya ukatili wa kijinsia…” Amesema James Sambuka.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *