TAASISI YA TULIA TRUST YATOA MSAADA WA KITI MWENDO, VENANCE ATUMA UJUMBE MZITO KWA DKT.TULIA ACKSON

Hii ni zaidi ya Upendo, mbio ya Bendera ya Upendo inayo kimbizwa na taasisi ya Tulia Trust ikibeba ujumbe wa Upendo, Mshikamano na Uwajibikaji imemfikia ndugu yetu Venance Enoss mkazi wa Kiwira wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Katika picha ni Venance Mwaisango akiwa amekaa katika kitimwendo alicho kabidhiwa na taasisi ya Tulia Trust kitakacho msaidia kutoka sehemu moja kwenda nyingine 10 Dec 2023.

Aidha pamoja na kupokea msaada huo Venance pamoja na wananchi wengine katika eneo la Kiwira wamemshukuru sana Dkt. Tulia Ackson amabaye ni spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kwa namna ambavyo amekuwa msariwa mbele katika kuwasaidia watu mbali mbaliwanao hitaji misaada wananchhi hao wameenda mbali zaidi na kusema Dkt. Tulia ni mfano wa kuigwa na viongozi wengine ili waendelee kufanya kazi kwa masrahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Kiongozi wa Mbio ya Bendera ya Upendo ambae ni Afisa Habari wa Tulia Trust Joshua Edward amewaasa Watanzania kuendelea kushikamana kuwa wamoja ikiwa ni pamoja na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan mara baada ya kufika kata ya Kiwira wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya kutoa msaada wa kiti mwendo kwa mhitaji. Huu ni muendelezo wa mbio ya Bendera ya Upendo ikihimiza Watanzania kuwa na Upendo, Mshikamano na Uwajibikaji

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *