Spika Dkt. Tulia akabidhi misaada kwa waathirika wa mafuriko Hanang, Ampongeza Rais Samia.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson leo tarehe 6 Desemba, 2023 ametembelea eneo lililoathirika kwa mafuriko na maporokoko ya tope na magogo Wilaya Hanang Mkoani Manyara na kukabidhi misaada ya bidhaa mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko hayo.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akikabidhi misaada kwa wahanga wa mafuriko Marakesh Mkoani Manyara yaliyo tokea Dec.03.2023

Bidhaa hizo zilizokabidhiwa kwa niaba ya Bunge la Tanzania na kupokelewa na Mhe. Jenista Mhagama Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera na Uratibu ni pamoja na Kilo 3000 za mchele, kilo 3000 za Unga Maharage kilo 800, mafuta ya kula lita 500, katoni 13 za sabuni pamoja na sabuni ya unga viroba 30.

Wakati huohuo Dkt. Tulia alipata fursa ya kuwatembelea na kuwapa pole waathirika wa mafuriko hayo wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo. Aidha, ameipongeza Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kutoa huduma za kibidamu kwa haraka hususan matibabu bure kwa wahanga hao.

Mara baada ya kupokea misaada hiyo, Mhe. Mhagama amempongeza na kumshukuru Dkt. Tulia na kwa namna ambavyo Bunge limeguswa na janga hilo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha misaada yote iliyotolewa inawafikia waathirika wote.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *