Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 6 Disemba, 2023 amewatembela na kuwajulia hali majeruhi wa maafa ya mafuriko ya matope na mawe yaliyotokea Wilaya ya Hanang ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.
Dkt. Tulia ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa uharaka na kazi nzuri ya kuhudumia majeruhi hao. Aidha ameipongeza timu ya madakatri waliotoka Mikoa ya jirani kufika mapema katika Hospitali ya hiyo kuongeza nguvu kwa ajili ya kuhudumia majeruhi hao.