Serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan kupitia Bohari ya dawa (MSD Medical Store Department) imemkabidhi Mbunge wa Kilolo Mhe. Justin Lazaro Nyamoga vifaa tiba kwa ajili ya vituo vitatu vya Afya vya Ruahambuyuni, Ilula na Nyalumbu vyenye thamani ya zaidi ya TZS Milioni 600.
Mhe. Nyamoga ameishukuru na kuipongeza Serikali kwa kutoa kibali cha kupatikana kwa vifaa tiba hivyo ambavyo vitaongeza kasi ya utoaji wa huduma za afya kwa Tarafa mbili za Mazombe na Mahenge kuptia vituo hivyo vitatu vya Afya.
Pia vifaa hivi vitapunguza kero ya wananchi wa maeneo hayo kwenda umbali mrefu hadi Iringa mjini kwa ajili ya kupata vipimo ambavyo awali havikuwepo kwenye maeneo yao ya kutolea huduma za afya.
Mhe. Nyamoga pia amewapongeza Bohari ya dawa (MSD) kwa kuongeza ufanisi na kurahisisha upatikanaji wa vifaa tibaikiwemo madawa kwa wakati na hivyo kuondoa adha ya upatikanaji wake na kuzorotesha upatikanaji wa huduma bora za afya.