MADAWATI YA JINSIA YUNDWA SHULENI KUKOMESHA UKATILI.

Kufuatia ongezeko la vitendo vya ukatili kushamili zaidi shuleni serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekutana jijini mbeya ili kuboresha mifumo ya kukupinga ukatili ikiwa ni pamoja na kuunda madawati ya jinsia katika shule za jiji hilo ili kukomesha ongezeko kubwa la vitendo hivyo kwa wanafunzi na kuwafanya waweze kutimiza ama kuzifikia ndaoto zao kwa ajiri ya maendeleo ya Taifa.

Kikao cha uboreshaji mifumo hiyo kikinda sambamba na uundaji wa madawti hayo kimefanyika tarehe 25,Aprili Mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya. Huku wadau ama wajumbe wa kikao hicho wakiwa ni Wizara ya maendeleo ya jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi maalum,Mahakimu,Waendesha mashitaka,Polisi dawati la jinsia,Afisa vijana Halmashauri,Afisa elimu kata,Afisa mipango Miji,Mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa,Afisa elimu sekondari,Walimu,wanafunzi na Waandishi wa Habari.

Bi.Ngowi akizungumza mara baada ya kika amesema kuundwa kwa madawati hayo katika s.hule ni kuhakikisha puia mwanafunzi mwenyewe anashiriki katika kukomesha vitendo vya ukatili badla ya kuichia serikali na jamii pekee kushughulikia suala hilikwani pia ni haki yake ya kushiki kwani wanapitia changamoto mbali mbali.

Aidha amesema utafiti uliofanywa na serikali mwaka 2011 ulionesha kuwa 60% ya ukatili kwa watoto unafanywa wawapo nyumbani huku 40% ya ukatili ukifanyika wawapo shuleni na mipango ya kudhibiti ukatili unaofanyika nyumbani lakini kwa upande wa huu unaofanyika shuleni tayali ushaanza kutokomezwa ikiwa ni pamoja uundaji wa dawali la jinsia shuleni ili kumsaidia mtoto ikiwa atafanyiwa ukatili aidha Nyumbani au shuleni kuripoti katika dawati na baadaye taarifa hizo kupelekwa kwa uongozi kama Afias maendeleo ya Jamii,Polisi dawati,ama uongozi wa shule kwaajiri ya kupatiwa msaada zaidi.

“Dawati litaundwa kwa kuchagua viongozi huku likisimamiwa na walimu wawili walezi wakike na wa kiume amabao watachaguliwa na wanafunzi wenyewe amabo wataona ni walimu rafiki na wenye Upendo kwao ili kuweka wepesi wa wanafunzi kuripoti mara wanapokumbana na changamoto ya Ukatili” Amesema Bi. Christabella Ngowi.

Amesema ili kuboresha usalma wa utoaji wa taarifa kila shule itakayo undiwa dawati itakuwa na sanduku la maoni amabalo ambalo litakuwa sehemu ya usiri ili kuyalinda maoni ama taarifa za wanafunzi lakini zaidi ni kumfanya mwanafnzi kuwa huru na kutohofia kuonekana pindi anaripoti taarifa za ukatili.

Kwa upande wake kamanda wa Polisi kitengo cha dawati la jinsia Loveness Mkama amesema vitendo vya ukatili kwa watoto vinapaswa kupingwa kwa kwani pamoja na kwamba wanaweza kufanyiwa wakiwa watoto wadogo lakini kumbukumbu ya vitendo hivyo inaendela kuaslia katika akili zao kitendo kinachoweza kupelkea matatizo mengine kama matatizo ya Afya ya akili na athari zake hazitaishia kwa mtoto tuu bali zitenda kuikumba familia nzima mfano kushuka kwa uzalishaji mali.

“Leo huii hapa tunazungumza masuala ya ukatili na afya ya akili lakini athari zake ni kubwa sana hivi unadhani ni mzazi yupi atakuwa tayali kwenda shamba ama kufanya shughului yoyote ile ya kiuchumi ikiwa mtoto wake atakuwa amebakwa ma kulawitiwa mwishowe jambo hili lita athiri mtoto,Mzazi na mwishowe Jamii nzima” Amesema kamanda loveness Mkama.

Wakizungumza mara baada ya kukamilika kwa uundaji wa dawati hilo walimu wameshukuru jitihada mbali mbali zinzofanywa na serikali pamoja na wadau ili kyukomesha vitendo vya ukatili kwa wanafunzi na kiuahidi kuyasimamia vizuri madawati hayo ili kulinda maadaili,utu,haki za mtoto na haki za binadamu kwa ujumla

Hamani Sumaka mwanafunzi wa kidato cha Tatu ameshukuru kwa uanzishwaji wa dawati hilo na kusema luitakuwa kipaza kwao ili kuripoti matukio ya ukatili hata huivyo amechaguliwa kuwa kiongozi katika dawali la jinsia katika shule ya sekondari Mponja atatumia uongozi wake kwakushirikiana na viongozi wenzake pamoja na wanafunzi wote kwa ujumla pamoja na walimu wenzake kuhakikisha wanamaliza tattizo la yukatili kwa wanafunzi shuleni hapo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *