WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII YAZITAJA NGUZO 5 ZA AJENDA YA NAIA.

Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia , wanawake na makundi maalum imebainisha Nguzo kuu 5 za Ajenda jumuishi iliyoandaliwa kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma rafiki za afya na kuondoa vikwazo vya maendeleo kwa vijana balehe nchini wenye miaka 10 – 19

Tafiti zinaonesha vijana balehe wanakabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwemo maambukizi makubwa ya VVU, mimba za utotoni, vitendo vya ukatili wa kimwili, kiakili na kisaikolojia, lishe duni, mdondoko katika shule za msingi na sekondari, na ujuzi duni wa kufikia fursa za kiuchumi.

Kikao cha uboreshaji mifumo hiyo kikinda sambamba na uundaji wa madawati hayo kimefanyika tarehe 29,Aprili Mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa shirika la DSW Halmashauri ya Arusha Jijini Arusha. Huku wadau ama wajumbe wa kikao hicho wakiwa ni Wizara ya maendeleo ya jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi maalum,Mahakimu,Waendesha mashitaka, Afisa elimu kata,na jeshi la Polisi,Waandishi wa Habari.

Wizara imezitaja Nguzo hizo kuwa ni kama ifuatavyo:

1.Kuzuia maambukizi ya VVU/UKIMWI Wizara imepanga kutoa huduma hii Kwa vijana na kuendesha huduma mbali mbali kama to hear Kwa vijana.

2.Kutokomeza Mimba za utotoni Kwa mujibu wa utafiti taarifa zilizo letwa na Serikali na wadau wa masuala ya wanawake na watoto zinaonesha kuwa hili jambo la Mimba za utotoni limekuwa tatizo hivyo zimewekwa taratibu kulimaliza katika jamii zetu.

3.Kuzuia Ukatili wa kijinsia. Kutokana na Takwimu zilizotolewa kutoka kwenye utafiti wa mwaka 2022/23 zinaonesha kuwa Hali ya ukatili wa kijinsia ziko juu sana Kwa Mkoa wa Arusha.

4.Kuboresha Lishe. Akifafanua wakati wa utoaji mada Bi. Christabella Ngowi amesema Nguzo hizo zinatwgemeana Kwani Moja ikiwa haiko imara basi nyingine haiwezi kuwa imara hivyo tujitahidi kuweka ubora Kwa kila Nguzo.

5.Akimalizia kuzitaja Nguzo hizo amesema uchumi ni kila kitu katika jamii yoyote hivyo wizara pamoja na wadau Wana shirikiana kuhakikisha Wanawajengea Uwezo wa kuzitambua na kuzikimbilia Fursa mbali mbali za kiuchumi.

Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2022, Tanzania Bara ina vijana 13,849,707 wa umri balehe (10-19) ambao ni ΒΌ ya idadi ya watu wote nchini ambao ni 59,851,347. Sensa 2012 vijana balehe 12,439,677,

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *