ELIMU ILIVYO ONGEZA TAKWIMU ZA MATUKIO YA UKATILI ARUSHA

Kwa mujibu wa takwimu za utafiti wa masuala ya ukatili wa kijinsia za mwaka 2022/23 zinaonesha kwamba bado ziko juu sana katika Mkoa wa Arusha kutokana na kuwa na idadi kubwa ya ripoti za matukio ya ukatili.

Je, hii inamaana kwamba Elimu imeifikia jamii sawa sawa Ama Elimu haijawafikia sawa sawa wananchi?

Bwn. Denis Mgiye Afisa ustawi Mkoa wa Arusha akifafanua hili amesema takwimu za miaka tatu 2021/22/23 za matukio ya ukatili zinaonesha 2021 jumla ya watoto 1118 waligangiwa ukatili huku wakike 804 na wakiume ni 314.

Mwaka 2022 jumla ya watoto 960 waligangiwa ukatili Me 330 huku jinsia Ke wakiwa 630.

Mwaka 2023 kulikuwa jumla ya matukio 918 kukiwa na mchanganuo ufuatao Me walikuwa 432 huku watoto wa jinsia ya kike kukiwa na ripoti ya matukio 486.

Mgiye amesema hizi ripoti zinahusisha ukatili wa kimwili na kingono katika Mkoa wa Arusha.

Baadhi ya wadau katika kikao cha Serikali na wadau Ili kuimarisha mfumo wa kupinga ukatili wa kijinsia wameingiwa na ukakasi kafuatia takwimu hizi.

Bwn. Mgiye amesema sio kweli kwamba mikoa ambayo taarifa na nmna hiiziko chini unamaanisha hakuna matukio ya ukatili bali sababu kubwa inayo pelekea takwimu hizi kuwa juukwa Mkoa wa Arusha ni kutokana na juhudi zinazo fanywa katika kutoa Elimu Kwa jamii kuzijua njia mbali mbali za utoaji taarifa pindi matukio haya yanapo tokea.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *