UIMALISHAJI MIFUMO YA KUZUIA UKATILI WA KIJINSIA WAJA NA NEEMA KWA VIJANA ARUSHA.

Ajenda mbali mbali zilizo jadiriwa katika Kikao cha kuimarisha Mifumo ya Kuzuia ukatili wa kijinsia kwenda kuwanufaisha Vijana lika na vijana balehe walioko ndani ya mfumo wa shule na walioko Nje ya mfumo rasmi wa shule Mkoani Arusha.Kikao hicho kimefanyika Aprili,30 Mwaka huu katika Ofisi za Taasisi ya Dustche Sturning Weltebevolkeburg (DSW) zilizoko Wilaya ya Arusha Mkoani Arusha na kuhudhuriwa na wadau mbali Mbali kama Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum,Jeshi la Polisi,Maafisa Elimu kata,Maafisa ustawi,Wanafunzi,Walimu wakuu wa shule,mwenyekiti wa SMAUJATA Mkoa,Afisa vijana ngazi ya halmashauri,Afisa ardhi na Polisi dawati la jinsia.

Akizungumza wakati wa kikao hicho bwana Jiriki Milingi ambaye ni Afisa tarafa ya Upoli akimwakirisha mgeni rasmi katika Kikao hicho amesema Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Ina tambua changamoto mbali mbali zinazowakumba vijana Ina andaa sera nzuri na mikakati ya kuwasaidia Vijana amesema Serikali inaendelea kushirikiana na wadau mbali mbali katika kishiriki na kutekeleza miradi mbali mbali Nchini ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Arusha.Aidha amiainisha ajenda hizo kitaiga kuwa ni pamoja na kuwekeza katika Afya na maendelao ya vijana barehe (NAIA-AHW) mwaka 2021/22-2024/25 inayozungumzia mpango wa Kuzuia maambukizi ya VVU/UKIMWI Kwa vijana lika na vijana balehe Nchini.Pia ameongeza kuwa mradi mwingine wa kuwakomboa vijana ni Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto (MTAKUWWA) Ili kukomesha ukatili wakijinsia ambapo Mkoa wa Arusha ripoti za matukio ya ukatili Kwa mwaka 2022/23 zimekuwa juu.

Kwa upande wake Mwakirishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Bi.Chiristabella Ngowi amesema wazazi/walezi hawatakiwi kubaki nyuma katika kupambana na ukatili Kwa kutumia vyema jukumu la malezi Kwa watoto wao hasa kipindi hiki qmbacho kumekuwa na wimbi kubwa la ukatili wa mtandaoni Kwa watoto na vijana nankuwakumbusha kuwa yapo mambo ya kuzingatia kukomesha wimbi hili.

1.Jenga uhusiano mzuri na mtoto juu ya masuala ya TEHAMA Ili mtoto ajue na luelewa matumizi sahihi ya mitandao

2.Anza kuzungumza mapema masuala ya Techinolojia na mtoto wako tangu angalia mdogo hii itamsaidia hata atakapo kuwa kijana kutambua faida na hasara za mitandao ya kijamii na teknolojia kwa ujumla.

3.Epuka kumpa maelekezo marefu mwanao kuhusiana na teknolojia Kwani ikifanya hivyo utamchanganya zaidi.

Kikao hicho kimehitimishwa kwa wizara na wadau kuunda madawati ya jinsia katika shule za Wilaya ya Arusha na kugawa vifaa vya Michezo,Televisheni,Spika na vipaza sauti Ili wanafunzi Ili wavitumie kukemea ukatili wawapo shuleni na nyumbani.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *