TENGENI MAENEO YA MICHEZO- WAZIRI MKUU TANZANIA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Khasim Majaliwa Majaliwa amewataka wakuu wa Mikoa kote Nchini kuwaagiza wakuu wa Wilaya zote kutenga maeneo ya wazi Kwaajiri ya wananchi na Wanamichezo kufanyia mazoezi.

Ameyasema hayo Mei 11siku ya kilele cha mbio za Mbeya Tulia Marathon zilizofanyika katika Uwanja wa kumbukumbu Sokoine Jijini Mbeya.

Aidha Majaliwa ameongeza kuwa mazoezi yanapofanywa hata Kwa muda mfupi tuu yanasaidia Kwaajiri ya kujenga mwili.

“Mazoezi sio lazima ukimbie Kilometa 5,10 au 15 ndipo ionekane umefanya mazoezi hata ukikimbia Kilometa 1 tuu inatosha sana lakini usikubali kukaa tuu bwete” Amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Khasim Majaliwa Majaliwa.

Kwaupande mwingine amesema Serikali inatengeneza mfumo mzuri Kwaajiri ya kuwafanya wananchi kote Nchini kushiriki katika mazoezi na hivyo inatazamia kutenga siku ya Jumamosi kama siku maalumu Kwaajiri ya wananchi kufanya mazoezi.

Na haya maeneo sio lazima iwe Barbara mnaweza kutenga kutokana na Fursa zilizopo katika maeneo yenu Ili wananchi wafanye mazoezi hayo Ili kuepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *