TGDC YA WASIHI WANANCHI KUTUMIA JOTOARDHI KUKABILANA NA MADILIKO YA TABIANCHI.

Kampuni ya Uendelezaji jotoardhi Tanzania TGDC imewasihi wananchi kutumia vyema nishati hiyo ili kukabiliana na madadiliko ya tabianchi yanayoendelea kuzikumba Nchi mbali mbali ulimwenguni.Hayo yamesemwa katika siku ya ufunguzi wa maonesho ya Mbeya Expro 2024 yaliyofanyiaka katika viwanja vya Uhindini jijini Mbeya ambapo yanatarajiwa kufanyika kwa siku Nane kilele chake kikitarajiwa kuwa 30. Mei.Mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa maonesho hayo Mjiokemisti na Mtafiti wa nishati ya joto ardhi Bwn. Ariph Kimani ameseama ziko njia mbali mbali za kutumia nishati ambayo haiathiri mazingira yetu huku moja wapo ikiwa ni nishati ya Jotoardhi ambayo inaweza kutumiwa kwa shughuli mbali mbali kama vile Kilimo cha mbogamboga na maua,Uvuvi,Utalii,Viwanda na utotoreshaji wa Vifaranga pamoja na shughuli zingine za kila siku bila kuharibu mazingira yetu.Amesema Jotoardhi ni chanzo kingine kimeongezeka katika kundi la mwanzo la vyanzo viwili vya uzalishaji nishati ya umeme ambayo ni maji na Gesi lakini upekee unaoambatana na chanzo cha jotoardhi ni kuwa hata endapo ukame ukitokea chanzo hiki kita endelea kuzalisha nishati na hakuna malighafi (Maji)inayo weza kupotea kwani hufanyika mchakato mzunguko wa Maji hayo Kwa ajiri ya kuanza upya mzunguko huo (Jadidifu).

Alipo kuwa akizungumza na waandishi wa habari Mwakirishi wa Mgeni rasimi katika maonesho hayo Juma Zuberi Homera kwaniaba ya waziri wa Viwanda na biashara ameseama siku chache zilizo pita Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia uluhu Hassan alizindua matumizi ya Nishati safi ikiwa ni njia moja wapo ya kukabilian ana mabadiliko ya tabianchi katika taifa letu.

Bwn.Kimani ameitaja baadhi ya miradi inayotekelezwa na kampuni hiyo kuwa ni pamoja na Mradi wa Ngozi uliyopo Rungwe, Kenyumbaka uliyopo Busokelo,Songwe uliyopo Mbozi,Luhio uliyopo Kibiti pamoja na miradi miwili yenye jina la Natroni iliyoko Mkoani Arusha.
Kwa upande wake Dkt. Keneth Lupogo Mkurugenzi wa huduma za ufundi katika kampuni hiyo amewataka wananchi wa Jiji la Mbeya na Maeneo jirani kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo na hasa katika banda la TGDC ili wapate elimu kuhusiana na Jotoardhi.

Maonesho haya yamehudhuriwa nawadau mbali mbali wakiwemo wadadu wa Nishati na viwanda kutoka Nchi jirani za Zambia na Malawi na makampuni mbali mbali pamoja na mashirika ili kuonesha bidhaa na huduma wanazotoa kwa jamii

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *