VIJANA 13,700 JIJINI MBEYA KUNUFAIKA NA MRADI WA “SAFA”.

Taasisi ya Deutsche Stiftung Weltbevolkerung (DSW) Kwa kishitikiana na Mashirika mengine kama KUNE na HRNS wamepanga kuwafikia vijana 13,700 katika mradi wa SAFA ambao umeshanza kutekelezwa na utatekelezwa mpaka mwakani 2024.

Vijana hao watanufaika na Elimu ya stadi za maisha,Elimu ya AFYA ya Uzazi Michezo na Burudani,Namna nzuri ya kupinga ukatili wa Kijinsia,kuwapa Elimu ya kuziona fursa za kijasiriamal na Elimu ya kuepuka matumizi ya Dawa za kulevya na kuepuka maambukizi mapya ya VVU /UKIMWI ambapo katika taarifa za utafiti zilizo chapishwa siku chache zilizo pita zilionesha Mbeya ni miongoni mwa mikoa mitatu yenye maambukizi zaidi ya VVU/UKIMWI DSW inaendesha mafunzo haya katika Mikoa minne ambayo ni Mbey,Songwe,Kilimanjaro pamoja na Arusha

Mkurugenzi wa shirika la DSW Tanzania Ndg: Peter Wago amewataka vijana kuchangamkia zaidi fursa za kiujasiriamali Ili Taifa letu liweze Kuendelea zaidi “Kundi la vijana ni kundi muhimu sana katika Taifa lolote lile na ndiyo maana hata ukiangalia mataiga ya mashariki yaliyo endelea (BIG ASIAN TIGERS) yanaonekana yameendelea Kwa sababu wame wekeza nguvu zao zaidi katika kundi hili muhimu la vijana” kwahiyo Kwa kulitambua hilo Vijana wa Mbeya wanaenda kuguswa na mradi huu ikiwa ni Kwa wale walioko katika mfumo wa shule na hata wale walioko Nje ya mfumo wa shule lengo letu ni kuwafikia vijana wote lakini Kwa kuanza tumeanza na vijana hawa 13,000 Kwa Jiji la Mbeya ambapo kata 10 kwa kila wilaya zitanufaika katika mradi huu.

Nusra Mushi mwakirishi na mkufunzi kutoka Wizara ya Afya Dodoma ana sema katika Yale ambayo vijana wa Mbeya watanufaika nayo ni pamoja na Afya ya Uzazi Kwa Ili tuwe na watu wenye Afya Bora ni lazima tulilenge kundi hili muhimu la vijana tunaenda kuwapatia Elimu vijana barehe wa miaka kuanzia 10-19 ambao Hawa wamegawanyika katika makundi makuu matatu Kuna kundi la Awali ambao ni miaka 10-13 kundi la Pili miaka 14-16 na kundi la tatu ni miaka 17-19 Aidha Bi.Mushi amesema Kuna haja kubwa sana ya kuwekeza katika kundi hili Ili tuepushe baadhi ya mambo kama Mimba za utotoni,matumizi hagifi ya njia za Uzazi,hatari ya kuambikizwa Magonjwa ya zinaa na ngono kama VVU.Hali hafifu ya kiuchumi na kutopata upatikanaji wa taarifa sahihi na Ushauri kuhusu Afya ya Uzazi.

Ndg.Kileo mwakirishi pia kutoka Wizara ya Afya Dodoma pia nasema matumizi ya Dawa za kulevya limekuwa Kwa kasi na ni jambo ambalo tunapoteza nguvu kazi ya Taifa Kwani tuna vijana wenye tatizo la Afya ya akili,wagonjwa,ongezeko la vitendo vya ukatili wa Kijinsia na madhara mengine mengi ambayo yanaweza kusababishwa na matumizi ya Dawa kama cocaine,bangi,marijuana,Pombe,caphein,gundi naHeroine.

Inspekta Loveness Mtemi kutoka jeshi la polisi mkoa wa Mbeya katika kitengo cha Daati la jinsia alishiriki mafunzo hayo na kuwaasa wananchi juu ya kuacha vitendo vya unyanyasaji na ukataili kwa vinachangia kwa kiasi kikubwa kuziolota na kurudisha maendeleo ya Nchi nyuma. Amewataka wanaanchi kuacha kuogopa jeshi la polisi kwani siku zote jeshi hilo liko kwaajiri ya kuwasaidia wananchi hivyo unapopata vitendo vya ukatili wa kijinsi ama unaposhuhudia mtu ambaye anafanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia mapema unapaswa kutoa taarifa katika jeshi la polisi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *