Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuimarisha mfumo wa kodi ulio rahisi kuutumia kwa kuwekeza zaidi katika mifumo ya kidijitali na kuwafikia walipa kodi wengi zaidi pamoja na kuimarisha ofisi za kodi kila Mkoa na Wilaya zake Zanzibar.Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo katika hafla ya Maadhimisho ya mwezi wa Shukrani na Furaha kwa mlipakodi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 29 Disemba 2023.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amempongeza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) Yusuph Mwenda kwa kuleta mabadiliko ya utendaji na ufanisi wa kuongezeka ukusanyaji mapato Zanzibar .Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha ZRA inapatiwa bajeti asilimia 100.Pia ameiagiza Wizara ya Nchi ofisi ya Rais Utumishi kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kukamilisha marekebisho ya stahiki ya mishahara ya watumishi wa ZRA.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amezindua mfumo mpya wa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya kodi ZIDRAS (Zanzibar Integrated Domestic Revenue Administration System).Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza wafanyabiashara wote wakubwa, wa kati na wadogo wa Unguja na Pemba walioshinda Tuzo za ulipaji kodi vizuri Zanzibar.

Also Visit Us on YouTube .BOMBAFMDIGITAL

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *