Ali Hassan Mwinyi afariki dunia

Rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, aliyeanzisha mfumo wa demokrasia ya vyama vingi katika taifa hilo la Afrika Mashariki, amefariki dunia Alhamis akiwa na umri wa miaka 98.

Tangazo la kifo cha rais huyo mstaafu limetolewa na rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan katika ujumbe uliorushwa moja kwa moja katika televisheni ya taifa hilo ya TBC.

“Ndugu wananchi, ni kwa masikitiko makubwa nakitangaza kifo cha rais mstaafu, aliyefariki saa kumi na moja na nusu jioni,” alisema Samia.

Rais Samia amesema mwinyi ambaye alihudumu kwa mihula miwili kama rais, amefariki kutokana na saratani ya mapafu. Mwaka jana mwezi Novemba, alilazwa katika hospitali moja mjini London ila akarudi mjini Dar es Salaam kuendelea na matibabu.

Tanzania sasa itakuwa na siku saba za maombolezo ya kifo cha Mwinyi huku bendera zikipeperushwa nusu mlingoti. Rais Samia ameongeza kuwa, kiongozi huyo aliyeleta mabadiliko ya kidemokrasia Tanzania, atazikwa hapo kesho Jumamosi.Mwinyi aliondoa vikwazo katika biashara za kibinafsi na kulegeza sheria za ununuzi wa bidhaa kutoka nje, jambo lililompelekea kupewa jina la utani, “Mzee Rukhsa.”

HISTORIA YAKE NA MWALIMU JK NYERE: Kambarage Nyerere kama mrithi wake, na alichukua uongozi wa nchi iliyokuwa katika mgogoro wa kiuchumi, kufuatia majaribio ya kisosholisti ya miaka kadhaa yaliyofeli.

Akiwa alizaliwa Mei 8, 1925 katika koloni la zamani la Uingereza lililoitwa Tanganyika, Mwinyi alihamia Zanzibar kusomea Uislamu. Babake alitazamia kwamba mwanawe atakuwa kiongozi wa kidini ila Mwinyi ambaye alikuwa kijana wakati huo, akawa mwalimu kabla kuingilia siasa katika miaka ya 1960 baada ya tanganyika kupata uhuru wake.

Kufuatia muungano wa Tanganyika iliyokuwa inajitegemea na Zanzibar uliopelekea kubuniwa kwa Tanzania mwaka 1964, Mwinyi alihudumu kama balozi wa Tanzania nchini Misri. Alihudumu pia kama waziri wa afya, masuala ya ndani na maliasili katika miaka ya 1970 na 1980.

Mwaka 1984, akawa rais wa Zanzibar kabla Nyerere hajamchagua kuiongoza Tanzania. Alipongezwa kwa kufungua milango ya demokrasia ya vyama vingi mwaka 1992 na kuvikubalia vyama vya upinzania kuwania nyadhfa katika uchaguzi, miaka mitatu baadae, alipoachia ngazi.

ALIKUMBANA NA LAWAMA WAKATI WA UONGOZI WAKE:

Alilaumiwa kwa madai ya kuwapendelea wafuasi wa dini ya Kiislamu katika uteuzi wake wa maafisa waandamizi serikalini, madai aliyokiri kwamba yalimtia uchungu.

Hata hivyo ukombozi wa kiuchumi uliofanyika wakati wa utawala wake uliandamwa na sakata za ufisadi, zilizokuwa mbaya kiasi cha kuwapelekea baadhi ya wafadhili kusitisha misaada kwa Tanzania mwaka 1994.Tangu kustaafu siasa mwaka 1995, kiongozi huyo aliyekuwa na nywele za kijivu, alikuwa haonekani sana katika majukwaa ya umma.Katika uzinduzi wa kitabu chake mwaka 2021, Rais Samia alimmiminia sifa tele, akimuelezea kama kiongozi anayestahili kuigwa. Katika kitabu hicho kuhusu maisha yake, Mwinyi aliukosoa “ujamaa” ulioanzishwa na Mwalimu Nyerere, akisema uliwanyima mapato wafanyabiashara wadogo wadogo.

NOTE: kwa makala nzima ya safari yake ya Maisha na uongozi usiache kutazama katika akaunti yetu ya youtube Bomba FM Digital

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *