JUKWAA LA WANAWAKE WA VIJIJINI WAPAZA SAUTI MWANAMKE KUTOMILIKI ARDHI.

Jukwaa lawanawake wa vijijini (RWA) wamepaza sauti kwa jamii na wadau kuwasaidia wanawake wa vijijini wananvyo nyimwa nafasi ya kumiliki Ardhi kitendo ambacho ni kinyume na haki za kibinadamu,Jinsia na Usawa.
Akizungumza wakati wa kuandaa mpango kazi wa uzinduzi wa kampeni ya MWANAMKE KUPEWA NAFASI YA UMILIKI ARDHI Mkurugenzi wa shirika la (MIICO) Bi. Catherine Mulaga ameseama ziko sababu nyingi sana ambazo zinapelekea mwanamke kunyimwa nafasi ya kumiliki ardhi ikiwa ni pamoja na Mila na desturi zisizo faa,Mfumo dume, Ukosefu wa elimu katika jamii.
Aidha Bi. Mulaga ameongeza kwa kusema kampeni hiyo itafanyika kwa mwaka mmoja itaisaidia sana jamii kufahamu na kuelewa umuhimu wa usawa katika umiliki wa Ardhi,kuacha mila na desturi zisizo faa,kuepusha migogoro na kukuza uchumi.

Bi. Catherine Mulaga Mkurugenzi wa shirika la (MIICO)

Kwaupande wake Afande Loveness Mtemi kamanda kutoka jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia Mkoa wa Mbeya amesema ukatili wa kijinsia unafanywa kwa kiasi kikubwa kwa wanawake wa vijijni ndiyo unaopelekea hata wanawake kunyimwa nafasi na uhuru wa kumiliki ardhi huku mwanamke akihusishwa wakati tuu wa kuanda mashamba huku ikiwa tofauti inapo fikia wakati wa mavuno.
“Mwanamke anaonekana anafaa na anamchango mkubwa wakati wa kuanda mashamba na hapo Mume anakuwa karibu sana na atamuita majina yote mazuri lakini inapofika wakati wa mavuno inakuwa tofauti Mume anatoka na kwenda kutumia na wanawake wengine huko nje” Amesema Afande Loveness Mkami

James Sambuka mtaalam wa msaada wa kisheria amesema kwa mujibu wa sheria kila mtu bila kijali jinsia yake anayo haki ya kumiliki ardhi bila kuvunja sheria na utaratibu .Amesema kuna ardhi amabazo zinakuwa zimetengwa kwa shughuli maalum mfano Ardhi ya Hifadhi mbali mbali na maeneo tengefu kwa ajili ya Michezo na kadharika hivyo pamoja na kwamba tuna haki ya kuimiliki ardhi bado tunapaswa kuyaheshimu maeneo hayo yanayo kuwa yametengwa kwa shughuli maalum.

Kwa upande wao maafisa ustawi ngazi ya Kata wamesema mara nyingi wanapokea zaidi malalamiko ya mogogoro ya ardhi hasa migogoro inayohusiana na mirathi na mara nyingi katika migogoro hiyo imekuwa ikihusisha wanawake kunyimwa nafasi ya kumili vipande vya ardhi mara baada ya wanaume zao kufariki familia ya marehemu huja juu na kudai ardhi ilikuwa ni umiliki wa mwanaume na hivyo kuonesha nia ya kuichukua kwa nguvu kutoka kwa mwanamke.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *